Hosted by Dailymotion. For legal issues report at the Copyright Center, report us on DMC, or use the Instant Removal tool.
Fadhy Mtanga - Alaa Kumbe!
2 Views • Nov 05, 2014
Description
Waanza kukuna kichwa,
Unawaza,
Utawaza sana!
Ukipata jawabu,
Heko nyingi.
Jana,
Hukuyamaliza yalojiri,
Ungeyamaliza vipi?
Uwezo hukuwa nao,
Kwa nini?
Najua huna jibu.
Maisha!
Kwani ni nini?
Ama yana nini?
Utawaza sana,
Nami nawaza sana,
Ala kumbe?
Kumbe nini?
Wajiuliza mara mia,
Uwape tena?
Lipi jipya litakuja?
Ngoja kidogo.
Maisha, maisha,
Yanakwisha,
Usiseme hivyo,
Nisemeni?
Sijui.
Hayo madaraka,
Tumewapa,
Wengine wakachukua bila kupewa,
Nini chanzo?
Pengine tamaa.
Tulikuwa na matarajio,
Eti eh!
Matarajio?
Ya nini tena,
Kwenu hamli?
Hapana.
Sasa nini?
Hali bora.
Alaa kumbe!
Ikawaje sasa?
Hatuhitaji kukujibu,
Maana hali yenyewe,
Mwenyewe si unaiona?
Hapana sioni kitu,
Ni kweli,
Huoni kitu ingawa una macho,
Machoyo mapambo,
Huwezi ona lolote,
Kwa kuwa,
Hupendi kufanya jitihada,
Jitihada? Za nini tena?
Katika kufikiri.
Mmh!
Sote tukaguna.
Fadhy Mtanga
http://www.poemhunter.com/poem/alaa-kumbe/
Keywords & Tags
More from User
Laxmy Alvarado - Sunlight
PoemHunter.com
Laxmy Alvarado - Sunlight
PoemHunter.com
Fatima Alzhara Rafa - Wholeness
PoemHunter.com
Fatima Alzhara Rafa - Wholeness
PoemHunter.com
Kaziah K - Eight Months Later
PoemHunter.com
Kaziah K - Eight Months Later
PoemHunter.com
Related Videos
Fadhy Mtanga - Lonesome Feelings
PoemHunter.com
Fadhy Mtanga - I'm So Sorry
PoemHunter.com
Fadhy Mtanga - Good Friendship
PoemHunter.com
Fadhy Mtanga - Utakuwa Wangu
PoemHunter.com
Fadhy Mtanga - Stay With Me
PoemHunter.com
Aisha Retno Alaa Alaa Ariana Grande | Gempak TV
Gempak